Canada:'Hatutawaachia magaidi watambe'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Canada Steven Harper

Mji mkuu wa Canada , Ottawa, umeingia matatani baada mashambulizi ya silaha katika majengo ya bunge. . Awali askari aliekuwa akilinda eneo la kumbu kumbu za vita vya dunia alipigwa risasi na kuuawa .

Mtu ambaye alipigwa risasi na kuuawa ndani ya bunge amefahamika kama Michael Zehaf-Bibeau.

Akizungumza kupitia televisheni Waziri mkuu wa Canada , Steven Harper amesema kuwa nchi yake haitatishwa na mfulurizo wa mashambulizi ya hivi karibuni ambapo askari mmoja aliuawa na bunge la taifa kuingiliwa na watu wenye silaha.

Bwana Harper amesema wataongeza mara dufu juhudi zao dhidi ya wale wanaotumai kuleta ukatili wao kwenye ndani ya Canada. Msako mkali wa usalama uliokuwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Ottawa, umesitishwa, licha ya kwamba maeneo yanayozingira bunge bado yamefungwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eneo la tukiso la shambulizi la kigaidi Canada

Bwana Harper amesema hatawaacha magaidi watambe.

Shambulio limekuja saa kadhaa baada ya Canada kukemea vikali vitendo vya kigaidi siku ya Jumatatu.

Vyombo vya usalama nchini humo vimethibitisha kuwa mshambuliaji mmoja ameuawa na ametambuliwa kwa jina la Michael Zehaf-Bibeau. Kufuatia tukio hilo waziri mkuu wa nchi hiyo Stephen Harper amehutubia Taifa hilo na kutaka wananchi watulie huku akisisitiza kuwa Canada haitowaachia magaidi watambe.

Shambulio limekuja saa kadhaa baada ya Canada kukemea vikali vitendo vya kigaidi.siku ya jumatatu mwanajeshi mwingine aliuawa katika shambulio la kushtukiza.