Obama asihi ukweli katika Ebola

Msafiri kutoka Sierra Leone akaguliwa kama ana Ebola uwanja wa ndege wa Chicago, Marekani

Chanzo cha picha, REUTERS

Rais Obama amewasihi Wamarekani kwamba wanapopambana na tishio la Ebola wasikilize ukweli, siyo uoga.

Katika hotuba yake ya kila juma, Rais Obama aliwasifu wakaazi wa jiji la New York kuwa wanaendelea na shughuli zao wakiwa shuwari baada ya kujilikana kuwa daktari mmoja aliyerudi mjini humo kutoka Afrika Magharibi, sasa anaugua Ebola.

Baada ya tukio hilo magavana wa New York na New Jersey wametoa amri kuwa mtu yeyote anayewasili kutoka Afrika Magharibi ambaye alikuwa karibu na wagonjwa wa Ebola - awekwe karantini kwa siku 21.

Serikali ya Rais Obama haikuwahi kutangaza hatua kama hiyo.