Afhanistan yakabidhiwa kambi kubwa

Kituo cha Bastion, kambi ya UIngereza, Afghanistan Haki miliki ya picha MOD

Kituo kikubwa cha jeshi la Marekani na Uingereza kusini mwa Afghanistan, kimekabidhiwa kwa askari wa usalama wa Afghanistan, miaka 13 baada ya majeshi wa kigeni kuingilia kati na kuipindua serikali ya Taliban.

Ni hatua muhimu katika utaratibu wa kupunguza wanajeshi wa nchi za magharibi nchini humo.

Kwenye sherehe iliyofanywa Kambi "Bastion", bendera za Uingereza, Marekani na NATO, zilishushwa huku muziki wa kijeshi wa Marekani ukichezwa.

Mwandishi wa BBC alioko huko anasema kwa vile wanajeshi 1,000 tu wa kigeni wamebaki, kambi hiyo kubwa sasa inaonekana kama imehamwa.

Wanajeshi wa Uingereza wanatarajiwa kuondoka Afghanistan ufikapo mwisho wa mwaka, lakini kikosi kimoja cha Marekani kitabaki.