Kobane yashambuliwa zaidi

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kobane ikifuka moshi kwa mashambulizi ya is.

Wapiganaji wanaouhami mji wa Kobane usishambuliwe na wanamgambo wa dola wa kiislam wameendeleza mashambulizi ya anga zaidi dhidi ya vikosi vya wanamgambo wa is waliokuwa kwenye msafara wenye vifaa mbalimbali kutoka eneo la Raqqa ambayo ni ngome yao.

Kuna taarifa kutoka katika mpaka wa Uturuki karibu na mji wa Kobane kwamba ukiwa maili kadhaa unaona moshi ukifuka kuelekea angani kiashiria kwamba wanamgambo wa dola ya kiislamu wanaendelea na mashambulizi yao dhidi ya mji huo.

Wiki iliyo pita wapiganaji wa angani wa kikurdi wakisaidiwa na nchi ya Marekani waliwarejesha nyuma wapiganaji hao wa dola ya kiislam hadi nje ya mipaka ya Kobane.