Mapigano makubwa yaua 130 Libya

Mapigano makubwa yamneshuhudiwa kati ya vikosi vya jeshi la Libya na wanamgambo wa dola ya kiislamu wakijaribu kuteka ngome kubwa ya kijeshi mashariki mwa mji wa Benghazi,imethibitishwa na maafisa wa jeshi la Libya.

Watu wapatao 130 wameuawa katika kipindi cha siku kumi zilizopita katika mapigano ya mtaani kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini humo miaka mitatu baada ya kuangushwa kwa utawala na kifo cha Muammar Gaddafi.

Mapigano mapya yanaripotiwa kutokea kati ya jeshi na kikundi cha Ansar –al-Sharia ambacho Marekani inakishutumu na kukishuku kutekeleza mauaji ya balozi wake mnamo mwaka 2012.

Watu kumi wameuawa baada ya vikosi vya Yemen kuwashambulia Al Qaeda katika mapigano makali kuwahi kutokea eno hilo.

Hali ya usalama katika mji huo wa Benghazi na maeneo mengine ya nchi ya Libya haijatengamaa kufuatia jeshi la nchi hiyo kushindwa kudhibiti hali ya usalama katika maeneo ambayo hapo awali yalikua yakidhibitiwa na jeshi la nchi hiyo.

Kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Libya bunge la nchi hiyo limepunguza bajeti yake kutokana na kushuka kwa ushuru wa mafuta ya nchi hiyo.

Balozi nchini nchini Libya zimeondoa wafanyakazi wake mpaka sasa kwa kuhofia usalama na maafa.