Tunisia yawachagua wabunge wapya

Image caption raia wa Tunisia wapiga kura

Raia nchini Tunisia wanapiga kura hii leo kwenye uchaguzi wa ubunge ikiwa ni karibu miaka minne tangu yafanyike mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Zine el-Abidine Ben Ali.

Mwandishi wa BBC kwenye mji mkuu Tunis anasema kuwa watu milioni tano wameandikishwa kama wapiga kura na pia kuna zaidi ya vyama 100 vinavyogombea

Msemaji wa tume ya uchaguzi nchini Tunisia anasema kuwa vituo vya kupigia kura vinalindwa na wanajeshi .

Uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika mwezi ujao.

Tunisia ndio imetajwa kama chimbuko la vuguvugu la kidemokrasi ambalo lilipanga kuondoa serikali za kiimla katika mataifa kadhaa ya kiarabu.

Hatahivyo makundi yenye itikadi kali yametishia kuvuruga uchaguzi huo na siku ya alhamisi wanamgambo walimpiga risasi afisa mmoja wa polisi viungani mwa mji mkuu wa Tunis.