Uchaguzi mkali watarajiwa Brazil

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dilma na Neves

Mamiloni ya wapiga kura nchini Brazil wataanza kupiga kura muda mfupi unoakuja katika duru ya pili na ya mwisho ya uchaguzi wa urais.

Waandshi wa habari wanasema kuwa hicho ndicho kinyanganyiro kikali zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadha nchini Brazil.

Kinyanganyiro hicho ni kati ya rais Dilma Roussef wa chama wa Workers party na Aecio Neves wa chama cha Brazilian Social Demoracy Party.

Waandishi wa habari wanasema kuwa matokeo yatategemea zaidi yule atakayeshinda kura kutoka maeneo ya viwanda vya kusini.

Watu maskini nchini humo bado wana imani na bi Roussef hususan kutokana na mipango yake ya kuwasaida huku matajiri wakimuunga mkono bwana Neves kwa matumani kuwa atainua uchumi wa nchi hiyo.