Vurugu Burkina Faso wakimpinga rais

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Blaise Compaore wa Bukina Faso

Kumetokea vurugu kubwa baina ya maelfu ya waandamanaji na maafisa wa polisi katika mji mkuu wa Burkina Faso wa Ougadougou, wakati maelfu ya raia wa nchi hiyo walipokuwa wakihudhuria mkutano kupinga marekebisho ya Katiba itakayomruhusu Rais wa nchi hiyo kuongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Maafisa wa usalama walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya wanadamanaji hao ambao walikuwa akiandamana kwenda kwenye majengo ya bunge.

Waandamanaji hao wanapinga kubadilishwa kwa katiba ya nchi hiyo ambayo itaotoa nafasi kwa rais Compaoure kugombea tena nafasi ya urais wa nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Hata hivyo kama ilivyotarajiwa katika maandamano kama haya maafisa wa polisi kama kawaida walikabilana na wanadamanaji hao kwa mabomu ya machozi.

Hadi sasa hakuna taarifa za watu waliojerehiwa au kupoteza maisha katika vurugu hizo.

Tayari vyuo vikuu, shule na maduka yalifungwa kwa wiki moja kabla maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa.

Rais Blaise Compaore alishika madaraka ya nchi hiyo baada ya kuipindua serikali tangu mwaka 1987 ambapo alichaguliwa katika kwa njia ya kidemokrasia kwa kipindi cha miaka miwili mwaka 2005.

Katika mahojiano na BBC hivi karibuni Rais Blaise Compaore aliwahi kusema kuwa atafanya mambo kwa maslai ya nchi hiyo.

Rais Compaire tayari ameshinda uchaguzi wa nchi kwa vipindi vinne. Hata upinzani umekuwa ukihamasisha raia kumpinga na kumlazimisha kuondoka madarakani ifikapo mwaka ujao.