Ebola na matokeo yake

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sierra Leone

Sierra Leone imeshutumu uamuzi wa nchi ya Australia kusitisha zoezi la kutoa visa kwa raia kutoka Africa Magharibi zilizo athiriwa na ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa habari wa Sierra Leone.Alpha Kanu ameielezea hatua hiyo kama ni ya kibabe na kibaguzi na kwamba haitazaa matunda.

Wakati huo huo msemaji wa serikali ya uganda ameshangazwa na namna nchi za Magharibi kwa ujumla wake wanavyo chukulia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Akaongeza pia kuwa nchi hizo zimejenga wasiwasi mkubwa kwa umma wa raia wa nchi za Africa Magharibi,na kwamba hii haitasaidi juhudi zinazofanywa za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ili kuudhibiti.