usalama pembe ya Africa na Ebola ukoje?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon na Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim wanakutana na Mwenyekiti wa Muungano wa Afrika AU hii leo kujadili mlipuko wa Ebola na masuala ya uslama katika mataifa ya pembe wa Afrika.

Bwana Ban na Jim pamoja na mashirika mengine ya kimataifa, wako katika ziara ya mataifa ya Ethiopia, Kenya na Djibouti kuangazia masuala ya maendeleo na amani. Tayari Umoja wa Mataifa na Benki ya dunia yametangaza ufadhili wa Dola bilioni nane, kusaidia mataifa hayo. Kwa sasa tuungane na mwandishi wetu Emmanuel Igunza akiwa jijini Addis Ababa.

Wakati huo huo ripoti mpya ya shirika la kutetea haki za binaadamu duniani limeishutumu serikali ya Ethiopia kwa mateso,kukamata raia na mauaji ya maelfu wa watu,ambapo nchi ya Ethiopia ni nchi yenye ukabila mkubwa na kabila kubwa ni Oromo.

Ripoti hiyo ambayo ilitolewa mapema jana inaeleza kwanza kabila hilo la oromo limeonekana kuonewa na kufikisha idadi ya watu wake 5,000 kukamatwa na kuwekwa korokoroni bila hatia yoyote na wengine wakipotelea kusiko julikana ama kuuawa kwasababu ya kuonekana ni wapinzani wa serikali ya nchi hiyo.