Wauaji wa Meyiwa kutambuliwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kelly Kumalo mpenzi wa Senzo akiwa na mtoto wa Senzo Meyiwa.

Polisi nchini Africa Kusini wameonesha nyuso zinazo dhaniwa kuwa ni wauaji wa golikipa na kapteni wa timu ya taifa Africa Kusini Bafana Bafana, Senzo Meyiwa.

Meyiwa alipigwa risasi na kufa siku ya jumapili wakati alipokuwa akikabiliana na wavamizi waloingia nyumbani kwa mpenzi wake Kelly Khumalo ambaye ni mwanamuziki na pia ni muigizaji,maziko ya Meyiwa yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Kifo cha mwanasoka huyo kimeonesha picha halisi ya kiwango cha uhalifu na matumizi mabaya ya silaha nchini Africa Kusini.

Africa kusini inatajwa kuwa moja ya nchi zenye matukio makubwa ya uhali,na kiwango cha uhalifu kinazidi kuongezeka siku hadi siku.

Mwanzoni mwa mwezi huu mwanariadha Oscar Pistorious alihukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake.