Chelsea yaibuka kidedea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Didier Drogba

Didier Drogba ameipa ushindi Chelsea wa mabao 2-1 dhidi ya Shrewsbury.

Mchezo huo wa kombe la ligi marufu kama capital one, umechezwa usiku wa kuamkia leo.

Timu kadhaa zilijitupa uwanjani ili kutafuta nafasi ya kuingia robo fainali yaligi hiyo katika ligi hiyo.

Mario Balotelli ametia chachu katika ushindi wa mabao 2-1 iliyoupata Liverpool katik mchezo dhidi ya Swansea City.

Mashabiki wa Fulham nao huenda walilala mapema baada ya kushuhudia timu yao ikipokea kichapo cha magoli 5-2 pale walipoialika Derby.

Bournemouth wakailaza West Brome kwa jumla ya mabao 2-1, huku Sheff Utd ikiibamiza MK Dons kwa ushindi wa mabao 2-1