Watu tisa wauawa na tembo Malawi

Image caption Tembo waua watu Malawi

Watu tisa wamekufa baada ya kukanyagwa na tembo nchini Malawi.

Kati yao hao waliokufa yumo msichana wa miaka nane.

Mwandishi wa BBC anasema matukio ya tembo kuvamia vijiji jirani na mbuga za wanyama sio mageni.

Hata hivyo hilo ni tukio la kwanza kwa tembo kuua watu wengi.

Walinzi katika mbuga ya wanyama ya Liwonde mashariki mwa nchi hiyo, wamesema tembo hao wanaodhaniwa kuvamia wilaya ya mashariki ya Machinga wametokea nchini Msumbiji.