Aleksandar Tonev- Celtic,adaiwa mbaguzi

Winga wa timu ya Celtic Aleksandar Tonev,amepigwa marufuku kusakata kabumbu mechi saba mfululizo, kwa kosa la kutumia lugha ya matusi yenye kuashiria ubaguzi wa rangi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24,hukumu yake inafuatia tukio linalomhusisha mlinzi wa timu ya Aberdeen aitwaye Shay Logan wakati wa michuano ya ligi kuu ya Scotland mwezi September.

Hata hivyo timu ya Celtic haikuridhishwa na adhabu hiyo hivyo wamedai kuwa watakata rufaa,huku wakishikilia msimamo kuwa Aleksandar ambaye ni raia wa Bulgaria si mbaguzi wa rangi.

Mchezaji huyo alihamia Scotland Champions kwa mkopo akitokea Aston Villa mwezi August na amechezea mechi kumi tu mpaka alipokwaa kisiki cha adhabu.

Naye msemaji wa timu ya Celtic ametoa kauli kuwa, ubaguzi wa rangi hauna nafasi katika mpira wa miguu,na wao kama kilabu na watu wengine wote,Celtic ni dhahiri kabisa inapinga ubaguzi wa namna yoyote.Na kuongeza kuwa wamepokea maelezo ya Aleksandar kwamba hakutamka maneno hayo,ambayo yanadaiwa ya kibaguzi na kuongeza kwamba yeye si mbaguzi na atakata rufaa juu ya adhabu yake.