Motisha juu wahudumu wa Ebola

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Gavana wa jiji la New York Andrew Cuomo

Serikali ya Marekani imeongeza fedha kwa wafanyakazi wa sekta ya afya wanaowahudumia watu walio athiriwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola ,lengo ni kuwavutia manesi na madaktari wengi zaidi kwenda kutoa huduma katika nchi za Afrika Magharibi.

Mpango huo umepata baraka zote za ikulu ya Marekani ,mbali na hayo wataalamu hao wa afya ambao watajitolea utaalamu wao , lakini pia wamehakikishiwa malipo manono,huduma za afya na kuhakikishiwa usalama wa ajira zao, pindi watakapo rejea nchini Marekani baada ya kazi.

Gavana wa mji wa New York Andrew Cuomo amesema changamoto ya ugonjwa wa Ebola inahitaji uwajibikaji wa kina wa dunia yote,ikiwemo kuwatia moyo wafanyakazi wa afya kutoka Marekani ili wakubali kwenda kutoa huduma za afya kwenye nchi zilizoathiriwa na ugonjwa wa Ebola.