Kambi ya jeshi yavamiwa Mombasa,Kenya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wanajeshi katika kambi

Wanajeshi katika kambi ya jeshi ya Nyali iliopo mjini Mombasa pwani ya Kenya wamewaua kwa kuwapiga risasi watu 6 baada ya genge la wahalifu kuvamia kituo hicho cha jeshi mapema leo.

Inadaiwa kuwa kundi la watu 15 lilijaribu kuvamia kambi hiyo mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ya jumapili.

Wanajeshi waliokuwa katika zamu waliweza kulidhibiti kundi hilo ambapo watu watano waliuawa huku askari mmoja akiweza kujeruhiwa kwa kukatwa na mapanga na wavamizi hao.

Kufikia sasa maafisa wa polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha shambulizi jilo.

Hatahivyo wengi wanashuku watu hao huenda ni wanachama wa kundi la Mombasa Republican Council MRC.

Lakini msemaji wa kundi hilo Randu Nzai amekanusha habari hizo akisema kuwa kundi hilo halikuhusika kamwe.