Maandamano zaidi yafanywa B-Faso

Mandamano ya Burkina Faso Haki miliki ya picha Getty

Jeshi la Burkina Faso limefyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji nje ya kituo cha utangazaji cha taifa katika mji mkuu, Ouagadougou.

Ripoti zinasema kuwa risasi zilifyatuliwa punde baada ya kiongozi wa upinzani, Sara Sereme, kuwasili pamoja na wafuasi wake.

Wanajeshi waliwatawanya maelfu ya waandamanaji waliokusanyika katika medani kuu mjini Ouagadougou.

Vyama vya upinzani vinataka iwekwe serikali ya muda ya raia hadi uchaguzi wa rais utapofanywa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa mjini humo, Mohamed ibn Chambas, ameonya kuwa Burkina Faso inaweza kuwekewa vikwazo iwapo jeshi litaendelea kuongoza nchi.