Viongozi wachaguliwa Donetsk na Luhansk

Haki miliki ya picha Other
Image caption Uchaguzi wafanyika katika maeneo ya Donetsk na Luhansk

Waasi wanaoiunga mkono Urusi mashariki mwa Ukrain hii leo wanafanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa kimaeneo na wabunge.

Kura hiyo ya maeneo yaliyojitenga ya Donetsk na Luhansk imelaaniwa na serikali ya Ukrain na viongozi wa nchi za Magharibi.

Mwandishi wa BBC mjini Kiev anasema kuwa haijulikani ni vituo vingapi vitafunguliwa au ni watu wangapi watapiga kura.

Maofisa wa eneo hilo wanasema kuwa hawana orodha ya wapiga kura.

Urusi tayari imesema kuwa itatambua matokeo ya uchaguzi huo.

Mapigano yanaendelea eneo hilo huku wanajeshi sita wa Ukrain wakiuawa na wengine 10 wakijeruhiwa tangu siku ya Ijumaa.