Jeshi kukabidhi nchi raia Burkina Faso

Image caption Luten Kanal Isack Zida wa Burkina Faso

Jeshi nchini Burkina Faso lililochukua madaraka ya nchi hiyo limesema litarejesha madaraka kwa wananchi kwa njia ya kidemokrasia .

Kiongozi aliyechaguliwa na jeshi hilo kuongoza kwa muda Luteni Kanali Isaac Zida amewaambia wanadiplomasia kuwa pande zote mbili zitashirikishwa katika mchakato wa kumpata kiongozi wa kudumu wa taifa hilo.

Hata hivyo mkutano wa viongozi wa bara la Afrika uliofanyika mjini Adis Ababa umetoa wito kwa serikali ya muda inayoongozwa kijeshi kukabidhi madaraka kwa wananchi ndani ya wiki mbili .

Hali ya utulivu imerejea katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou kufuatia machafuko ya wiki iliyopita ambayo yalisababisha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Blaise Compaore kuachia madaraka baada ya kuwa madarakani kwa miaka 27.