IS waua zaidi ya watu 300 Iraq

Haki miliki ya picha
Image caption wapiganaji wa Islamic State

Maofisa wa serikali nchini Iraq wamesema wapiganaji wa Islamic State wameua watu zaidi ya 300 wa madhehebu ya Sunni ambao wamekuwa wakipigana na kundi hilo katika jimbo la Anbar.

Waziri wa Iraq wa masuala ya haki za binadamu amesema kuwa miili zaidi 50 ikiwemo ya wanawake na watoto ilikutwa ikielea katika visima.

Hata hivyo vyanzo kutoka jamii ya Al-Bu Nimr vimeerifu kuwa kumekuwa na mauaji kwa awamu tatu tangu alhamisi wiki iliyopita maeneo mbalimbali ya Iraq wakiwemo wale wanajitoa mhanga katika mabomu.

Mashambulizi zaidi yanatarajiwa kwa waumini wa dini ya Shia katika sherehe za za Ashura.