Hamilton amshinda Rosberg,Langa Langa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Lewis Hamilton,Mercedes

Dereva Lewis Hamilton wa timu ya Mercedes amemshinda mwenzake wa timu hiyo Nico Rosberg katika mashindano ya langa langa ya US Grand prix.

Daniel Ricciardo wa timu ya Red Bull ameshika nafasi ya tatu baada ya kuendesha vizuri dhidi ya madereva wa timu ya Williams. Kwa ushindi huo Hamilton sasa anaongoza kwa pointi 24 mbele ya Rosberg huku zikiwa zimesalia duru mbili na uwezekano kupata pointi 75 Timu ya Mercedes imetawala mashidnano ya langa langa ya mwaka huu tofauti na miaka mingine.