Sunderland yainyuka Crystal Palace 3-1

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sunderland vs Crystal Palace

Steven Fletcher amefunga mabao mawili na kuisaidia timu yake ya Sunderland kuinyuka Crystal Palace 3-1 kwenye dimba la Selhurst Park na kujitoa kwenye shimo la kushukia daraja la ligi kuu ya England.

Katika mchezo huo pekee wa jumatatu usiku Fletcher aliifungia timu yake bao la kuongoza kabla ya mlinzi wake Wes Brown hajaisawazishia Palace kwa bao la kujifunga mwenyewe. Sunderland waliongeza mapigo pale Jordi Gomez alipoutia wavuni mpira kwa kombora la chini kabla ya Mile Jedinak hajatolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya njano ya pili kutokana na mchezo mbaya. Ushindi huo umemaliza mwendo mbovu wa Sunderland katika ligi hiyo baada ya hivi karibuni kuambulia vichapo mfululizo na sasa wamepanda hadi nafasi ya 15 na kuziacha shimoni Leicester City, QPR na Burnley…