Rais Poroshenko apinga uchaguzi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Petro Poroshenko

Rais Petro Poroshenko wa Ukraine amesema kuwa hatambui uchaguzi unaoendelea katika baadhi ya maeneo ya Mashariki mwa nchi hiyo na kwamba kwa hatua hiyo wanarudisha nyuma jitihada za kuleta amani nchini humo.

Katika hotuba yake iliyoonyehswa kwenye Runinga pia Poroshenko amesema kuwa serikali yake haitatambua upigaji kura huo katuika majimbo ya Donetsk and Luhansk.

Hata hivyo amesema kuwa hali ya machafuko katika mashariki mwa taifa hilo kumesababisha kuvunjika kwa hali ya amani na kuleta vurugu.

Poroshenko amesema kuwa anataraji kupendekeza sheria itakayopiga marufuku waasi kuanzisha katika eneo ambalo limepitishwa na kuwa eneo lenye harakati za kutaka kuleta amani.