Boko Haram washambulia Nigeria

Haki miliki ya picha a
Image caption Boko Haram

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram, wanashukiwa kuhusika katika shambulizi jingine huko mji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Shambulio hilo lilitokea wakati wa mchana Nafada na kuharibu kituo cha polisi, benki na ofisi ya chama tawala cha (PDP).

Mashahidi wa tukio hilo wanasema waliona miili ya wanajeshi watano. Kiongozi wa dini ya kiislamu wa eneo hilo ameuawa pia.

Mwandishi wa BBC anasema wanamgambo wa kundi hilo wamevamia maeneo mengi nakufanya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kuzidi kuanguka kutokana na mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo yanakuja siku baada ya kulipuliwa kwa bomu la kujitoa muhanga katika jimbo la Yobe na kuuwa zaidi ya watu kumi na tano.