Rais wa Ukraine aahidi mabadiliko

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Rais wa Ukraine Petro Poroshenko

Rais Petro Poroshenko, Ukraine ameitaka idara ya usalama na bunge la nchi hii kuiondoa sheria inayoruhusu kujitenga kwa maeneo mawili yaliyopo Mashariki mwa nchi hiyo.

Akizungumza muda mfupi baada ya mkutano wa baraza la usalama la nchi hiyo Poroshenko amesema amewaagiza baadhi ya makamanda kupeleka vikosi vyao katika eneo hilo ili kujikinga na mashambulio katika eneo hilo.

Amesema kuwa upo uwezekano wa waasi wanaosaidiwa na Urusi kuweza kufanya mashambulizi katika mji wa pili kwa ukubwa wa Kharkiv na Bandari ya Mariupol.

Hata hivyo hatua hii ya Rais Poroshenko inakuja huku siku ya jumapili waasi wa mashariki wa Ukraine walifanya uchaguzi katika majimbo ya Donetsk naJamhuri ya Luhansk.

Ukraine nan chi za Mahgharibi wametangaza kuwa uchaguzi huo si halali lakini Urusi inaonekana kuegemea kwa waasi hao Zaidi.