Real Madrid yailaza Liverpool 1-0

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Benzema akishangilia goli dhidi ya Liverpool

Katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imepigwa michezo minane ikiwemo ile ya mabingwa watetezi Real Madrid ambao wameinyuka Liverpool bao 1-0 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid.

Mfaransa Karim Benzema aliipatia Madrid bao hilo pekee baada ya kazi nzuri ya Marcelo.

Katika mchezo huo kocha wa Liverpool Brendan Rodgers alifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kwa kuwaweka nje wachezaji wake muhimu saba akiwemo nahodha Steven Gerrard, Rahim Sterling na Mario Balotelli.

Huko mjini London Arsenal wakiwa Emerates wameshindwa kulinda mabao yao pale waliporuhusu nyavu zao kutikiswa na kujikuta wakiambulia sare ya mabao 3-3 na Anderletch ya Ubelgiji.

Hadi dakika ya 60 ya mchezo vijana hao wa Arsene Wenga walikuwa mbele kwa mabao 3-0 kabla wageni hao hawajacharuka na kurudisha mabao yote na kumuacha Wenga amefura kwa hasira.

Kwingineko Borusia Dotmund wameikung’uta Galatasaray mabao 4-1, Juventus wakiiangushia kipigo cha 3-2 Olympiakos,kwenye mchezo wa mapema Bayer Leverkusen ya Ujerumani kuishushia kisago Zenit St Petersburg ya Urusi cha mabao 2-1 .

Hii leo Manchester City itashuka dimbani kumenyana na CSKA Moscow kwenye dimba la Etihad, Ajax Amsterdam na Barcelona ilhali Bayern Munich watacheza na AS Roma…na huko Ufaransa Paris St Germain watakwaruzana Apoel Nicosia ya Cyprus