Chanjo ya Ebola yatolewa Mali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafanyakazi wa afya Mali kupata chanjo ya Ebola

Kundi la wafanyakazi wa afya nchini Mali leo wanapewa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

Hii ina maana kwamba watu waliojitolea kufanyiwa chanjo ya majaribio nchini Mali kufikia watu 40.

Utafiti ulianza Mali kufuatia majaribio salama kufanyika nchini Uingereza na Marekani.

Chanjo hiyo imetengenezwa na wanasayansi katika Taasisi ya Taifa ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza huko Maryland, nchini Marekani na inatengenezwa na kampuni ya dawa ya Uingereza ya GlaxoSmithKline.

Kutokana na kupamba moto kwa maambukizi ya Ebola, Afrika Magharibi, kasi ya kupata chanjo inaendelea.