Watu 10 wauawa katika mlipuko Nigeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mlipuko katika eneo la bauchi nchini Nigeria

Ripoti kutoka kaskazini mwa Nigeria zinasema kuwa watu kadhaa wameuawa na mlipuko wa bomu karibu na mashine ya kutoa pesa ya ATM.

Walioshuhdia walisema kuwa ,mwanamume mmoja alikaribia watu waliokuwa wamepanga foleni kwenye mashine hiyo kwenye mji wa Azare ulio katika jimbo la Bauchi .

Walisema kuwa mwanamme huyo alikuwa amebeba bahasha ambayo baadaye ililipuka.

Siku ya Jumatano watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram walivamia kiwanda kimoja cha saruji ambapo walichukua baruti wanayotumia kwenye milipuko.