Tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika

Katika siku nne zijazo wachezaji 5 bora watakaowania tuzo ya BBC ya mchezaji bora Afrika mwaka wa 2014 watatangazwa.

Mbali na wachezaji hao nyota watano, kuna maina ya wachezaji wengi tu chipukizi ambao ndio bado wananoa vipaji vyao katika vilabu mbalimbali barani ulaya ambao nao wanapaswa kutambuliwa.

BBC Michezo imewaorodhesha hapa wachache ambao wameonesha kuwa watakuwa wakusifika katika siku sijazo.<span >

Image caption Nabil Bentaleb

NABIL BANTALEB

<span >Alitemwa na kilabu yake ya nyumbani,Lile akiwa na miaka 15 ,aliondoka na kujiunga na kilabu ya Mouscron nchini Ubelgiji kabla ya kujiunga tena na kilabu nyengine ya Dunkerque katika divisheni ya tatu.

Na baada ya kutemwa na kilabu zote tatu ni wakati huo ambapo meneja wa kilabu ya Tottenham Harry Rednapp alimuona mnamo mwaka 2012 ambapo maisha yake yalibadilika.

Wiki mbili baada ya kufanyiwa majaribio,aliandikisha mkataba na Spurs na kuanza kazi iliomfanya kushiriki katika ligi ya Uingereza,mechi za kuwania mataji ya ulaya pamoja na kushiriki katika kombe la dunia.

Alijiunga na kilabu ya Tottenham wakati Tim Sherwood alipoteuliwa kama meneja.

Sherwood amefanya kazi na Bentaleb katika timu ya vijana ya Tottenham kabla ya kumjumuisha katika timu kubwa na kuichezea timu hiyo dhidi ya Southampton mwaka 2013.

Tangu wakati huo, mchezo wake wa kasi ,pasi nzuri na kuimarika kwake kumemfanya kupata sifa kubwa kutoka kwa wenzake pamoja na wasimamizi wa timu hiyo.

Na alipozidi kuimarika Bentaleb alianza kuyavutia mataifa mengi .

Akiwa mzaliwa wa Ufaransa kutoka kwa wazazi ambao ni raia wa Algeria,mchezaji huyo wa miaka 19 alilazimika kuamua kati ya mataifa hayo mawili kabla ya kuamua kujiunga na Desert Fox ya Algeria.

Mnamo mwaka 2014 ,Bentaleb aliichezea timu ya Algeria kwa mara ya kwanza dhidi ya Slovenia katika mechi ya kirafiki.

Akianza katika safu ya Ulinzi katika kiungo cha kati na kuwafurahisha wengi na mbinu zake,pamoja na mchezo wake kwa jumla.

Bentaleb alifunga bao lake la kwanza katika mechi ya kirafiki ya kombe la dunia dhidi ya Romania.

Nchini Brazil Bentaleb alicheza kila dakika ya mechi za Algeria katika kundi lake,lakini hakujumuishwa katika mechi dhidi ya Ujerumani ambapo timu hiyo ilishindwa.

Na katika ligi kuu ya Uingereza Bentaleb alianza msimu huu pale alipoachia na mkufunzi mpya wa Totenham Mauricio Pochettino akichaguliwa mbele ya wachezaji mahiri.

Serge Aurier

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Serge Aurier

Akiwa na miaka 21,Serge Aurier tayari ametajwa kuwa beki bora wa safu ya nyuma upande wa kulia nchini Ufaransa.

Mzaliwa wa Ouragahio nchini Ivory Caost ,Aurier alielekea nchini ufaransa kama kijana mdogo ili kujiunga na wazazi wake katika eneo la Seine-saint-Denis ,katika kijiji kimoja cha mji mkuu wa Paris.

Mara ya kwanza kuonekana kama mchezaji ilikuwa katika kilabu ya nyumbani ya RC Lens.

Alipanda kupitia timu za vijana na alipofikisha umri wa miaka 17 alianza kucheza soka ya kulipwa katika ligi ya daraja la pili nchini humo.

Mchezo wa Aurier ulionekana kuwa bora katika soka ya kilabu hiyo.

Msimu uliofuata alishiriki katika mechi 31 za kilabu hiyo ka ligi ya daraja la kwanza.

Image caption Serge Aurier akigaagaa chini baada ya kuangushwa katika mechi kati ya Ivory Coast na Cameroon

Mchezo wake ulioimarika ulimuuza na hivyobasi kujiunga na kilabu ya Toulouse mnamo mwezi January mwaka 2012 huku aking'ara kusini magharibi mwa ufaransa na kuonyesha uwezo wake wa kulinda lango na kutamba na mpira katika safu ya kiungo cha kati na ile ya upande wa kulia.

Hatua hiyo ilivivutia vilabu kadhaa vya ulaya mbali na kuwavutia wachaguaji wa kikosi cha soka cha Ivory Coast.

Mnamo mwezi juni mwaka 2013,aliichezea timu ya taifa dhidi ya Gambia na kuonekana kama mrithi wa Emmanuel Eboue.

Alichaguliwa katika kikosi cha timu ya Ivory Coast cha kombe la dunia na alikuwa nyota katika kikosi hicho cha nchini Brazil.

Akiwa katika safu ya ulinzi,mchezaji huyo pia amekuwa akitoa pasi zilizosababisha mabao katika mechi dhidi ya japan ambapo aliwapigia krosi safi washambulizi Wlifried Bony na Gervinho ili kufunga mabao yalioiweka timu hiyo kidedea kwa mabao 2-1.

Mshambuliaji wa miaka mingi wa Ivory Coast Didier Drogba alimtaja bekio huyo kama bora zaidi nchini Ufaransa baada ya mechi hiyo.

Maumbile ya Aurier yanamfanya kuwa mchezaji msumbufu kucheza naye,ni mchezaji anayeweza kuumiliki mpira kwa mda ,ana kasi na anajua kuusoma mchezo.

Akiwa na maarifa ya kucheza mchezo wa kushambulia ngome ya wapinzani,hakutengeza mabao sita pekee bali pia alikuwa miongoni mwa wafungaji wa Toulouse akiwa na mabao sita msimu uliopita.

Hatahivyo yeye hucheza rafu mara nyeingine na ameweza kupewa kadi za nyano 11 msimu uliopita.

Baada ya kombe la dunia ,Aurier alijiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint Germain akiwa mkopo kutoka Toulouse.

Lakini amebaini kwamba maisha ni magumu dhidi ya PSG na anajua kwamba huenda kazi yake ikaathirika.

Anatarajia kujiunga na kikosi cha kwanza cha timu hiyo ili kuwashawishi PSG kumsajili katika kandarasi ya kudumu mwishoni mwa msimu huu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vincent Aboubakar

Vincent Aboubakar

Ameibuka kuwanawiri katika kipindi kifaacho zaidi

Aboubakar mwenye umri wa miaka 22 ameibukia kuwa mshambulizi wa kutajika na hata kuvutia klabu ya ya Porto iliyomsajili majuzi.

Mchezaji huyo wa Cameroon alishuhudia timu yake ikisajili matokeo duni katika kombe la dunia huko Brazil mapema mwaka huu jambo lililopelekea nahodha wa the Indomitable Lions <span ><span >Samuel Eto'o kustaafu.

<span >Chipukizi huyu alithibitisha umahiri wake aliporuhusiwa kurithi nafasi yake Etoo.

<span >Tayari Aboubakar amefunga mabao matatu kaatika kampeini ya the Indomitable Lions ya kufuzu kwa fainali ya dimba la Afrika mwakani.

Mchango wake katika timu ya taifa imemplelekea kukonga nyoyo za mashabiki wengi wa Cameroon tangu mwaka wa 2010 aliposajiliwa katika timu ya taifa ilipokuwa ikielekea Afrika Kusini katika kombe la dunia akiwa na miaka 18.

<span >Japo hakucheza Aboubakar alionesha wazi talanta yake.

<span >Punde baada ya kutajwa katika timu ya taifa alipata uhamisho kutoka<span >Coton Sport, hadi Valenciennes ya Ufaransa.

Wachambuzi wanasema talanta yake ilidumaa katika kipindi cha miaka mitatu aliyokuwa Ufaransa lakini punde alipohamia <span > Lorient Julai mwaka uliyopita talanta yake ilinawiri tena.

<span >Mshambulizi huyo alinoga na hata kufunga mabao 17 katika mechi 37 alizocheza .

<span >Umahiri huo ulimhakikishia nafasi katika timu ya taifa huko Brazil.

<span >Katika kipute hicho alicheza katika mechi mbili na kuwavutia mawakala wa vilabu kadha ikiwemo klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ya Hull City.

<span >Aboubakar aliamua kuelekea Ureno ambao tayari ameifungia timu yake ya Porto mabao 2 baada ya kucheza katika mechi 4 za ligi .

Mshambulizi huyo atakuwa Ureno kwa kipindi cha miaka minne.

Tunamtarajia Aboubakar kuendelea kutia fora uwanjani.