Ni akina mama au wasichana wenye bidii?

Image caption Utafiti unasema kuwa akina mama hufanya kazi kwa bidii ikilinganishwa na wanawake.picha ni kwa mujibu wa gazeti la nation nchini kenya.

Utafiti mpya unasema kuwa wanawake waliojifungua wanafanya kazi kwa bidii zaidi ya wasichana wasio na watoto.

Utafiti huo uliofanyiwa kampuni ya Microsoft ulishirikisha wanawake 2000 na waajiri 500.

Swali la utafiti huo lilikuwa ni nani kati ya wanawake wenye watoto na wasichana ambao hufanya kazi kwa bidii.

Nusu ya waajiri hao ambayo ni asilimia 57 walibaini kwamba akina mama ni wafanyikazi bora ikilinganishwa na wanawake wasio na watoto.

Karibia thuluthi moja ya asilimia 29 ya waajiri ilibani kwamba wafanyikazi wao wanafanya kazi kwa bidii baada ya kupata watoto huku asilimia 35 ikisema maarifa ya wafanyikazi hao huimarika wanapopata watoto.

Ijapokuwa waajiri wengi huona mda unaotumiwa na akina mama hao kuwanyonyesha wanawao kama gharama,mashirika yalio na sera kama hizo yamebaini kwamba utendakazi wa akina mamao hao umeimarika.

Kwa mfano, mwanamke ambaye ametoka kujifungua hutumia mda wake mwingi kazini ili kulipa mda aliopoteza.

Epimach Maritim,mkuu wa kitengo cha ajri katika kampuni ya G4s nchini kenya anakubali kwamba kwa kuwa akina mama wana sababu ya kuishi na kutumikia, hutumia mda wao mwingi kufanya kazi.