Adhabu ya kinyama kwa mwanamke India

Haki miliki ya picha savita verma
Image caption Mwanamke aliyeburuzwa na Punda baada ya kuokolewa na polisi

Mwanamke mmoja magharibi mwa India ameadhibiwa kwa kuburuzwa na Punda akiwa nusu utupu adhabu iliyoamrishwa na baraza la kijiji,Panchayat.

Uso wa mwanamke huyo ulikua umepakwa rangi nyeusi wakati alipokuwa akiadhibiwa.

Polisi inawashikilia watu takriban thelathini wakihusishwa na tukio hilo la kumdhalilisha mwanamke huyo mwenye umri wa miaka arobaini na mitano,tukio lililotokea baada ya mwanamke huyo kushutumiwa kumuua binamu yake.

Familia ya mwanamke huyo iliuchoma mwili wa binamu aliyedaiwa kuuawa na mwanamke huyo kabla ya kutoa taarifa kwa polisi.Afisa katika jimbo la Rajasthan ameiambia BBC kuwa ni kinyume cha sheria kwa baraza hilo kutoa hukumu ya namna hiyo.