Nuklia:Shaka kuhusu juhudi za Iran

Image caption Mazungumzo kuhusu mradi wa nuklia wa Iran nchini Oman

Mazungumzo ya siku ya pili kuhusu mpango wa Nuclear wa Iran yatafanyika baadaye Oman, wakati wapatanishi wakijaribu kupata makubaliano ya kina kabla ya muda wa wiki mbili uliokuwa umewekwa kukamilika.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry na mpatanishi wa Muungano wa ulaya , Catherine Ashton, atakutana tena na waziri wa mambo ya nje wa Iran , Javad Zarif.

Jumapili Rais Obama alikuwa amesema kuwa bado kuna pengo kubwa katika mpango wa majadiliano ya kimataifa kuhusu Nuclear na Iran na ametilia shaka ikiwa mpango huo utafaulu.

Rais Obama amesema kuwa suala tata ni kuhusu hatua kubwa iliyopiga Iran na ratiba ya kuondoa vikwazo.

Swala kuu zaidi katika mchakato huu ni ukubwa wa mradi wa kurutubisha madini ya Uranium na ratiba ya kuondoa vikwazo dhidi ya Iran.

Rais Obama alirejelea kuwa cha muhimu hapa ni kuhakikisha kuwa Iran haitaweza tena kutengeza zana za kivita, ila kwa maslahi ya wananchi.

Iran inasema mahitaji yake ni makubwa.

Rais Obama pia alisisitiza kuwa Marekani na Iran wana adui mmoja ambaye kundi la wapiganaji wa Islamic State, lakini alisema kuwa tatizo tu ni kwamba juhudi zao dhidi ya wapiganaji hao bado hazitoshi .