Israel hali si shwari

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wa Ki Israel huko West Bank

Mwanamke mmoja mwenye asili ya Israel ameshambuliwa kwa kisu na kusababisha kifo chake katika eneo la ukingo wa magharibi, tukio hilo limedumu kwa saa moja baada ya askari mwenye asili ya Israel pia kushambuliwa na kuumizwa vibaya mjini Tel Aviv.

Polisi wametoa taarifa kwamba washambuliaji wote na majeruhi hao ni raia wa Palestina.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi kutumia kila mbinu ili kukomesha kabisa mashambulizi hayo.

Inasadikika kwamba mashambulio ya namna hii yamesababishwa na suala la kuendelea kuwepo kwa mpango wa makazi mashariki mwa Jerusalem na suala la haki ya kuabudu katika eneo nyeti la msikiti wa Al Aqsa ulioko mjini Jerusalem ambao pia hujulikana kama hekalu la milimani.