Wembley Don yavurugwa

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Nyasi za Wembley Don zikitimbwa

Mkurugenzi mkuu wa uwanja wa Wembley Don Roger Maslin amesema kuwa uwanja huo kwa sasa hautakuwa katika viwango vinavyokubalika kimataifa kwa michezo.

Kauli hii inafuatia timu za mchezo wa ragby kukwaana katika uwanja huo wa mpira kitendo ambacho si cha kawaida, timu za mijibaba yenye nguvu na kushi barabara za Uingereza na Slovenia walipimana ubavu katika uwanja huo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kiongozi wa timu ya Uingereza Roy Hodgson wiki iliyopita alihoji juu ya uamuzi wa kuruhusu timu hizo mbili kukwaana katika uwanja huo siku sita tu kabla ya michuano ya kombe la uropa kuwania taji la mwaka 2016 haijaanza.

Nyasi za uwanja huo zimeng'oka na umevurugwa vilivyo baada ya wanaume hao kubingiritana kwenye nyasi hizo kati ya Dallas Cowboys na Jacksonville Jaguars na ndipo Masline anaposema kwamba kwa sasa nyasi za uwanja huo haziko sawa kama inavyostahili.

Kutokana na hali hiyo iliyojitokeza imefanikiwa kumvuruga vilivyo mkurugenzi huyo wa uwanja ingawa amebaki na tumaini moja tu ya kuwa uwanja huo utarejea katika hali yake ya kawaida mwezi wa tatu mwakani muda mfupi tu ujao wakati wa majira ya baridi.