MSF:Mbinu mpya zahitajika kukabili Ebola

Image caption Wafanyakazi wa afya wakitoa huduma kwa waathirika wa Ebola

Mbinu mpya mbalimbali zinahitajika kwa ajili ya kupambana na virusi vya Ebola nchini Liberia, shirika la madaktari wasio na mipaka, MSF limeeleza.

Zaidi ya Watu 6,000 wameathiriwa na ugonjwa huo nchini Liberia lakini takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya maambulizi mapya imeendelea kupungua.

MSF imesema kuwa imekuwa na uwezo mkubwa wa kuwa na vituo vingi vya kupambana na maradhi hayo kuliko idadi ya wagonjwa.

Mfano kituo kimoja mjini Monrovia kilikua na vitanda 250 lakini kimekua kikitibu wagonjwa 50 pekee, hivyo shirika hilo limeomba kubadilishwa kwa mbinu za mapambano dhidi ya ebola

Liberia ni nchi iliyoathirika zaidi na ugonjwa wa Ebola kwa karibu ya nusu ya idadi ya walioathiriwa wa ugonjwa huo Afrika magharibi.

Hivi sasa kiasi cha maambukizi kinaendelea kuwa juu nchini Guinea na Sierra Leone