Mshukiwa wa mauaji ya Meyiwa aachwa huru

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nahodha wa timu ya Bafana Bafana Senzo Meyiwa

Meyiwa alianza kuichezea Orlando Pirates mwaka 2005 kisha akawa nahodha wa timu ya Bafana Bafana.

Mahakama nchini Afrika kusini imetupilia mbali madai dhidi ya mtu aliyekamatwa akihusishwa na mauaji dhidi ya Senzo Meyiwa.

Zanokhule Mbatha alikamatwa na kikosi maalum mwezi uliopita.

Mahakama ilitoa amri ya kuachiwa kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha wa kumfanya Mbatha ashtakiwe.

Meyiwa aliuawa nyumbani kwa mpenziwe mjini Vosloorus,mashariki mwa Johannesburg.

Watu wawili wanadaiwa kuvamia nyumba ya Kelly Khumalo tarehe 26 Mwezi Oktoba na kudai simu za mkononi kabla ya kumfyatulia risasi Meyiwa.

siku moja baada ya shambulizi, Polisi nchini Afrika kusini walitangaza zawadi ya kitita cha dola 23,000 kwa atakayetoa taarifa na kutoa picha za watu wawili wanaoshutumiwa kumuua Meyiwa.