Maafisa kodi wacharuka Argentina

Image caption Miongoni mwa taasisi zilizokumbwa na operesheni hiyo.

Mamlaka ya kodi nchini Argentina imefanya operesheni dhidi ya taasisi zinazotakatisha fedha.

Maafisa wa kodi nchini humo wamefanya msako wa ghafla katika zaidi ya taasisi 70 za kifedha mjini Buenos Aires na katika majimbo mengine nchini humo.

Operesheni hiyo iliyofanywa katika taasisi hizo za fedha, imeelezwa na maafisa hao kwamba imelenga kukamata taasisi zinazotakatisha fedha.

Operesheni hiyo pia imeyakumba maduka ya kubadili fedha za kigeni.

Mzunguuko haramu wa fedha, umekuwa ukiathiri kwa kiasi kikubwa benki kuu ya Argentina, hasa katika fedha za kigeni.