Ujerumani mwiba kwa wanariadha

Image caption Dawa ya wanariadha Ujerumani yaja

Kwa mara ya kwanza Ujerumani imeamua kuweka sheria kali kwa wafukuza upepo kama kosa la jinai na atakaye patikana na hatia ya utumizi wa dawa za kuongeza nguvu atakabiliwa na adhabu ya kali ya lupango miaka mitatu .

Inakadiriwa wanariadha mahiri wapatao 7,000 ambao hukabiliwa na zoezi la upimaji, sheria hiyo inawaangukia na wanariadha wa kigeni nao hawatapona, watakabiliwa na kifungo.

Mapendekezo hayo ya sheria yatakabidhiwa kwa mawaziri wenye dhamana kabla ya kuanza kwa bunge la nchi hiyo mwakani