Netanyahu na Abbas katika malumbano tena

Haki miliki ya picha AFP y Reuters
Image caption Viongozi wa Israel na Palestina

Waziri Mkuu wa Israel amemlaumu kiongozi wa Mamlaka ya Palestina kwa kuchochea machafuko.

Benjamin netanyahu amesema Mahmoud Abbas anachochea ghasia mpya kwa rai aliyoitoa kuwa israel inasababisha eneo hilo kuingia katika vita vya kidini.

Rais Netanyahu amesema Bwana Abbas amekuwa akiwafundisha watu wake ugaidi zaidi, kushinda amani na kusema kuwa Israel inajaribu kumaliza machafuko kwa kuweka adhabu kali na kusambaza wanajeshi zaidi.

Katika ghasia zilizotokea siku mbili zilizopita raia wawili wa Israel na Mpalestina mmoja waliuawa.