Ebola: Hasara kubwa kwa Kenya Airways

Image caption Shirika la Kenya Airways lilisitisha safari zake katika baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi kutokana na mlipuko wa Ebola

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways linasema limepata hasara ya dola milioni 116 katika kipindi cha nusu mwaka kinachomalizika mwezi huu wa Novemba.

Shirika hilo linasema hasara hiyo imetokana na mlipuko wa Ebola katika nchi tatu za Afrika Magharibi na kuzorota kwa hali ya usalama.

Mwandishi wa BBC aliyefuatilia taarifa hiyo Emmanuel Igunza anasema kuwa huu ni mwaka wa pili kwa kampuni hiyo kurekodi hasara. Idadi ya wasafiri imepungua mwaka huu kutokana na taarifa kuhusu hali mbaya ya usalama nchini Kenya.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Mbuvi Ngunze anasema utendaji wa shirika hilo pia uliathiriwa na kusitishwa kwa safari za ndege katika mataifa ya Sierra Leone na Liberia -chi ambazo ziliathiriwa zaidi na Ebola.

Katika kipindi cha kati kati ya mwawezi wa Augost, Kenya Airways ilitangaza kuwa imesitisha safari zake katika nchi hizo mbili Safari hizo bado hazijafufuliwa .

Ngunze ameonya kuwa mapato ya kampuni hiyo yanaweza kushuka hata zaidi kama shirika hilo litaendelea kusitisha safari hizo.

Lakini si kampuni hiyo tu iliyoathiriwa na mlipuko wa Ebola katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guniea.

Shirika la ndege la Ethiopia, Ethiopian Airlines pia hivi karibuni lilisema kuwa mapato yake yameshuka hadi kwa kiwango cha asilimia 20 kufuatia hofu ya wasafiri juu ya Ebola.