Mabomu mawili yalipuka Libya

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Misri imelaumiwa kwa kuchochea mashambulizi hayo kutokana na harakati zake dhidi ya makundi ya kiisilamu

Habari kutoka katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, zinasema kuwa mabomu mawili ya kutegwa ndani magari yamelipuliwa , moja karibu na ubalozi wa Misri na jingine karibu na ubalozi wa milki za kiarabu .

Balozi zote hizo mbili zimefungwa kwa miezi kadhaa .

Hakuna taarifa kuhusu majeruhi kufuatia mashambulizi hayo.

Makundi ya kiislam yanayodhibiti mji mkuu awali yaliishutumu Misri kwa kuanzisha mashambulizi ya anga dhidi ya vikosi vya kiislam nchini Libya , shutuma ambazo zimekabushwa na serikali ya Misri.

Wakati huo huo Misri imeyashutumu makundi ya wapiganaji ya Libya kuwasaidia wapigganaji wa kiislam wa Misrui katika rasi ya Sinai