Shell yadaiwa ilipuuza onyo Nigeria

Image caption Mafuta yaliyovuija yaliathiri mazingira na kusababisha watu kuapoteza kazi

Mawakili wanaoiwakilisha jamii ya watu walioathiriwa na uchafuzi wa mazingira anasema wakuu wa kampuni ya mafuta ya Shell walijulishwa mapema kuhusu kuchakaa kwa mabomba yake ya mafuta.

Hii ilikuwa kabla ya kutokea kwa visa vya kumwagika mafuta mara mbili hivyo kuchafua pakubwa eneo hilo Lagoniland Kusini mwa Nigeria mwaka 2008.

Shell inakana kwamba ilikuwa na taariifa kuwa mabomba hayo yalihatarisha usalama.

Shell inadai mabomba hayo yalipasuliwa na wezi wa mafuta lakini mawakili hao wamejibu kwamba mabomba hayo yalikwa duni na yalimwaga mafuta hata kwenye ziwa la eneo hilo ambako sasa uvuvi haufanyiki tena.

Mafuta ya kwanza yalivuja mwaka 2008 Kusini mwa Nigeria kulingana na mawakili wanaoishitaki Shell.

''Shell inakataa kabisa madai kuwa iliendelea kuharibu mazingira kwa kujua licha ya kuarifiwa kuhusu hali chakavu ya mabomba yake,'' taarifa ya kampuni hiyo ilisema.

Ujumbe wa barua na barua pepe zilizowasilishwa mahakamani kuonyesha kuwa Shell ilikuwa na taarifa ya kuharibu mazingira ila ikapuuza tu zinaonyesha kuwa maafisa wakuu wa Shell walikuwa na wasiwasi kabla ya kuvuja kwa mafuta mara mbili kwani mabomba hayo yalikuwa yamechakaa sana.

Mafuta yalivuja katika eneo la Bodo mjini Ogoniland ambako watu waliohojiwa na shirika la Amnesty International walielezea athari walizopata kutokana na kuvuja kwa mafuta ikiwemo, kuumwa na kichwa na kuwa na tatizo la kuona.

Kutokana na kuvuja huko bei ya Samaki ilipanda mara dufu kulingana na shirika la Amnesty. Wavuvi walilazimika kutafuta kazi nyinginezo huku kukiwa na wasiwasi kutokana na kemikali zilizopatikana katika mafuta ambazo zinasemekana kusababisha Saratani.