Watoto wafundishwa kuweka akiba UK

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kanisa la Uingereza limetangaza mpango huu kuwafanya watoto kuwa na nidhamu ya pesa

Inaelezwa kuwa watoto wadogo hata walio na miaka minne wana nafasi ya kuunda vikundi vidogo vidogo vya kujiwekea akiba ili kuepuka kuwa na madeni katika maisha yao ya baadae.

Kanisa la nchini Uingereza limependekeza kuundwa kwa mtandao wa vilabu mashuleni,vilabu vinavyoendeshwa na taasisi za mikopo,ili kusaidia kuwapa uelewa watoto kuhusu maswala yahusuyo fedha.

Mipango hiyo, itawasaidia watoto kutunza kiasi kidogo cha fedha.

Pia watapata nafasi za kusimamia vikundi vyao wenyewe, kama vile kufanya kazi kama makarani wadogo wa fedha au mameneja wa benki.

Wazazi na wafanyakazi wa shule pia wanaweza kujiandikisha kwenye vikundi hivyo kwa ajili ya kuwa na akaunti za kuweka fedha kwa ajili ya gharama mbali mbali kama safari na sare za shule.

Mafunzo haya yaliyopendekezwa yatagusa maeneo kama ya uelewa kuhusu kazi ya fedha kwenye maisha ya watu, namna ya kutuza na kudhibiti pesa na namna ya kupambana na athari zinazosababishwa na pesa.