Equitorial Guinea kuandaa dimba

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa shirikisho la soka barani afrika Issa Hayatou

Taifa la Equitorial Guinea ndilo litakaloandaa michuano ya dimba la mataifa ya Afrika mwaka 2015.

Kulingana na shirikisho la soka barani Afrika, taifa hilo limetajwa baada ya Morrocco kukataa kuandaa michezo hiyo kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Morrocco ilikuwa imeiomba CAF kuahirisha dimba hilo la January 17 hadi Feruary 8.

CAF vilevile imeipiga marufuku Morrocco kushiriki katika dimba hilo ambalo sasa litaandaliwa na taifa lililoandaa kombe hilo na Gabon mwaka 2012.

Image caption Kombe la michuano ya bara Afrika

Equitorial Guinea sasa itachukua jukumu lote la kuandaa michuano hiyo yenye mataifa 16.

CAF imetangaza kuwa mechi hizo zitachezwa katika miji minne ikiwemo Malabo,Mongomo na Ebebiyin.Droo ya mechi hizo itafanyika mjini Malabo tarahe 3 mwezi Disemba.

Haijabainika iwapo mwenyeji huyo mpya atashiriki katika dimba hilo kwa kuwa timu hiyo ilipigwa marufuku mwezi Julai kwa kuchezesha mchezaji asiyetakikana katika mechi ya kufuzu kwa dimba hilo dhidi ya Mauritania mnamo mwezi May 17.