Watoto wazungumza lugha isiofahamika

Haki miliki ya picha Getty Image
Image caption Watoto wamekaa na mamayao wakila chakula.nchini Uganda watoto watatu waliofungiwa na baba yao kwa miaka saba wameanza kuzungumza lugha isiofahamika.

Watoto watatu kutoka kijiji cha Barca katika kaunti ndogo ya Aber Wilayani Oyam nchini Uganda wameanza kuzungumza lugha tofauti isiojulikana baada ya kufungiwa katika nyumba kwa miaka saba.

Lugha hiyo mpya imetajwa kuwa Leb -adam ikimaanisha lugha ya ubongo na jamii ya eneo hilo.

Inadaiwa kuwa baba ya watoto hao aliwafungia ili kuwalinda kutokana na hatari yoyote.

Kulingana ma gazeti la the monitor nchini Uganda,watoto hao hawajaathirika kiakili lakini hawawezi kuzungumza na watu wengine.Wanaamini tu kile baba yao anachowaambia.

Kulingana na mama yao watoto hao waliweza kuishi kwa kula mayai ya chura yaliochemshwa na majani,ambayo hula kila asubuhi na jioni na hutumia maji kutoka shimo lililochimbwa na baba yao.

Mama yao anasema kuwa baba ya watoto hao alimzuia kutozungumza nao hatua iliowafanya kutojifunza lugha ya kiluo wakati walipokuwa wadogo.

Mwanamke huyo amesema kuwa alionywa na baba huyo kutosema chochote kuhusu watoto hao.