Betri ya chombo Philae yaisha nguvu

Haki miliki ya picha ESA
Image caption Chombo Philae ambacho kimetua katika nyota mkia hakiwezi tena kurekodi data kwa kuwa betri zake zimeisha nguvu.

Chombo cha anga za juu Philae kilichotua katika nyota mkia kimetuma tena data nyengine mda mfupi kabla ya kupoteza nguvu za umeme.

Kila kilichotarajiwa kutoka kwa chombo hicho kilipokelewa kabla ya kuonyesha kwamba nguvu za battery za chombo hizo zimekwisha.

Chombo hicho kimezibwa na mwamba na hakiwezi kupata mwanga wa jua ili kuchaji battery yake.

Wahandisi wanahofu kwamba huenda data iliopatikana ndiyo ya mwisho kwa mda huu.

Chombo hicho kilitua katika sakafu ya nyota mkia siku ya jumatano,ikiwa ni mara ya kwanza kwa chombo kilichotumwa katika anga za juu kutua katika nyota mkia.

Fursa nyengine ya kuwasiliana na Philae ni wakati chombo cha Rosetta kilichopeleka Philae katika nyota hiyo kitaonekana tena.

Huku Philae ikiweza kupata mwanga wa jua kwa takriban jisaa moja na dakika hamsini pekee, haijulikani iwapo battery yake itaweza kupata nguvu ya kuendelea kutoa data.