Katika G20 Putin aonywa aondoke Ukraine

Waziri mkuu wa Australia,  Tony Abbot na Rais Putin wamebeba koala Haki miliki ya picha AFP

Viongozi wa mataiifa ya magharibi wanaohudhuria mkutano wa mataifa tajiri, G-20 mjini Brisbane, Australia, wameionya Urusi ifuate makubaliano ya kusitisha mapigano Ukraine, ama sivyo itakabili vikwazo zaidi.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alimwambia Rais Putin kuwa uhusiano baina ya Ulaya na Urusi utabadilika iwapo wanajeshi wa Urusi watabaki Ukraine.

Rais Obama alisema hatua za Urusi zinachusha.

Urusi inakanusha kuwa ina wanajeshi wake ndani ya Ukraine.

Msemaji wa Bwana Putin alitoa maanani ripoti kuwa kiongozi wa Urusi anapanga kuondoka mapema kwenye mkutano.