Kikao cha bunge chatibuka Somali

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kikao cha wabunge wa Somali Chatibuka mjini Mogadishu.kikao hicho kilitarajiwa kujadili hatma ya waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed

Kwa mara ya pili katika kipindi cha juma moja ,kikao cha wabunge wa Somali kilichoitishwa ili kuijadili hatma ya waziri mkuu nchini humo kimeisha kwa kelele na ghasia.

Wabunge walitarajiwa kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed ,lakini wafuasi wake walikataa kukaa na kuanza kuimba na kubeba mabango.

Bunge la Somali limelemazwa na mgogoro uliopo kati ya waziri mkuu na rais Hassan Sheikh Mhamud.

Marekani imesema kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani haina maslahi ya raia.

Umoja wa mataifa nao umesema kuwa una wasiwasi kuhusu ufisadi wa ununuzi wa kura unaokabili kura hiyo.