Kura dhidi ya waziri mkuu yapigwa Somali

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aliyekuwa rais wa Somali kushoto na waziri mkuu wa sasa nchini Abdiweli Sheikh Ahmed

Wabunge nchini Somalia wanapiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed.

Shughuli za bunge zimekwama kutokana na tofauti zilizopo kati ya waziri kuu na rais wa Somalia Hassan Sheik Mohamud.

Wadadisi wanasema kuwa hali imedhoofika kutokana na mizozo ya kisiasa.

Marekani inasema kuwa kura hiyo ya kutokuwa na imani haiwakilishi maslahi ya raia.