Watu 18 wakamatwa kwa ufisadi Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia waandamana Brazil kupinga ufisadi serikalini

Polisi nchini Brazil wamefanya uvamizi kwenye majimbo sita katika oparesheni kubwa ya kuchunguza ufisadi kwenye kampuni ya mafuta ya serikali ya Petrobras.

Watu 18 walikamatwa wakiwemo wakurugenzi wakuu wa makampuni makubwa ya ujenzi nchini brazil wanaoshutumiwa kwa kutoa hongo ili kujishindia kandarasi za pesa nyingi za kampuni hiyo ya mafuta.

Mkurugenzi wa zamani wa Perobras Renato Duque pia alikamatwa kwenye oparesheni hiyo iliyowajumuisha zaidi ya polisi 300.

Uchunguzi huo ulianza mapema mwaka huu wakati mkurugenzi mkuu wa zamani wa kampuni hiyo ya mafuta aliposema kuwa moja ya idara za kampuni ililipa mamilioni ya dola kwa wanasiasa wakiwemo wanachama wa chama tawala cha workers party.